Skip to content Skip to footer
Loading Events

« All Events

 • This event has passed.

GOLDEN JUBILEE CELEBRATONS (Parokia ya Kikambala 18Th May 2024)

May 18

PROGRAM

0900 :  Arrival of invited Guests

10.00 : Start of Holy Mass

Entrance Hymn &  opening Prayer

Pentential Rites & Gloria

Readings-   Somo la 1-

Wimbo wa Katikati

Somo la 2-

Injili

Kipaimara

Sala za waumini-

Sadaka

Sala ya Ekaristi

Komunio

Sala baada ya Komunio

Wimbo wa Shukurani

matangazo

1200: Baraka na Wimbo wa Mwisho

       

Nyimbo za Misa

Mwanzo-        

   TWENDENI KWAKE MUNGU  By Mwahunga James Munga   Key G

Twendeni kwake Mungu (Twendeni kwa Mungu),

 kwa shangwe na ndereme (Shangwe na nderemo);

Kwa kinanda na nyimbo tukamwabudu, na kayamba na ngoma tukamwabudu x 2

 1. Nyumbani mwa Mungu tuingie kwa shangwe, kwa nyimbo za sifa tumwabuda.
 2. Ni Mungu muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo.
 3. Na kila mwenye pumzi amsifu Mungu, na kila kiumbe kimsujudie.
 4. Aliyetuumba anatupenda, aliyetukomboa atupenda.
 5. Ni kwa upendo wake twajazwa neema, kwa wema wake twasamehewa.

 

Kumekucha – B.Mukasa  Key G

1.Kumekucha-ni sikukuu ya ajabu leo hii x2

Watu wote-wanameremeta tazama,

       Wamevaa-mavazi mazuri  oneni

        Nyuso zao-tabasamu shangwe nderemo na vifijo

2.Twimbe  wote-ni sikukuu ya ajabu leo hii

Tufurai-….

3.Mungu wetu…………..Katukuka………

4.Katupenda…………….Katuinua…………

5.Pendo gani………….Ametupa……..

6.Raha tele……………Mustarehe………..

          

 

 

  NJOONI TUINGIE    Key G  David Okoth Onyango

1.Njooni tuingie nyumbani mwa Bwana-Njooni tuingie nyumani mwake

Wazee ingieni nyumbani mwa Bwana-Njooni tuingie nyumbani mwake

 Tunaingia-kwa vifijo na shangwe,                      Kwa ngoma safi- na madaha na maringo

 Tujiandae-tuombe radhi kwa Mungu                 Atutakase-tukamtolee sadaka.

2.Vijana furahieni ulinzi wa Mungu-njooni tumshukuru Mungu wetu

Pamoja tujongee tupige makofi-njooni tumshukuru mlinzi wetu

3.Mwenyezi atupenda kwa pendo la kweli-njooni tumsujudu Muumba wetu

Kwa kweli tumeumbwa kwa mfano wake-njooni tumsujudu muumba wetu

 

   Chetezo         BWANA AMENITUMA Bruno S.Mpepo   Key A

Bwana amenituma kuwahubiri mataifa, Bwana amenituma mimi x2

Bwana amenitia mafuta kuhubiri habari njema x2

1.Roho wa Bwana yu juu yangu,kwa maana amenipaka mafuta,kuwahubiri masikini habari njema.

2.Amenituma kutangaza kufunguliwa kwao wafungwa  nao vipofu kupata kuona tena

3.Kuponywa waliovunjika moyo kuwafariji wote waliao kuwapatia maua badala ya jivu

               

 BWANA : MISA MILLENIUM  -Key G   John Mwendwa

    Bwana  Bwana Bwana utuhurumie x2

Kristu Kristu [Kristu] utuhurumie x2

Bwana  Bwana Bwana utuhurumie x2

 

UTUKUFU :

1.Utukufu kwa Mungu juu mbinguni Na amani duniani-Kwa watu aliowaridhia

     Tunakusifu,tunakuheshimu,tunakuabudu,tunakutukuza

2.Tunakushukuru kwa ajili, Ya utukufu wako mkuu- Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni

 1. Mungu Baba Baba mwenyezi, Ee Bwana Yesu Kristu Mwana pekee Ee Bwana Mungu.

4.Mwanakondoo wa Mungu Mwana wa Baba, Mwenye kuondoa dhambi, za ulimwengu utuhurumie.

5.Mwenye kuondoa dhambi, dhambi za ulimwengu, pokea ombi letu

 1. Mwenye kuketi kuume kwa Baba. Utuhurumie kwa kuwa ndiwe, uliye pekee yako mtakatifu

7.Pekee yako  Bwana pekee yako, uliye juu kabisa Yesu,Yesu Kristu.

 1. Pamoja na-Roho mtakatifu, katika utukufu, wa Mungu Baba Amina.

 

Bible Procession-

UZURI WA YESU Alfred Ossonga   Key C   T/S   2/4

Kwa imani yangu matendo na maneno, nihubiri neno la Mungu siku zote,

Nipeleke neno la Mungu pande zote, mataifa wanangojea neno hilo x 2

1.Kwa ajili yake Yesu Kristo Bwana wangu, kwa ajili ya uzuri wake wa Daima,

Uzuri wake Yesu usio na kiasi, nitende yote mema nifanane na Yesu

 1. Kwa ajili yake Yesu Kristo Bwana wangu, nimeyasahau maneno ya zamani,

Ya kale yamepita shetani ameshindwa, nimempata Yesu natembea na yeye

3.Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu, Kwa ajili ya uzuri wake wa daima,

nakaza mwendo sana nipeleke ujumbe, ujumbe wake Yesu kwa amataifa yote.

 

Somo la 1.                                          Mdo: 2, 1-11

Somo Kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume.

Ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi. Ukaijaza nyumba yote  waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za motouliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kusema kwa lugha , kama Roho alivyowajalia kutamka.

Na kulikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika,  wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapedokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia,Misri na pande za Libia karibu na Kirene , na wageni watokao Rumi. Wayahudi na Waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.

Neno la Mungu- Tumshukuru Mungu.

 

Wimbo wa katikati                                             Zab. 104; 1,24,29-31, 34.  K-30

         Waipeleka Roho yako-Venas Lujinya  Key D

     Waipeleka Roho yako, Ee Bwana Ee Bwana,

     nawe waufanya upya uso wa nchi-Aleluya

1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,Wewe Bwana Mungu wangu, umejifanya mkuu sana

    Ee Bwana jinsi yalivyo mengi matendo yako,Dunia imejaa mali zako.

2.Waiondoa pumzi yao wanakufa na kuyarudia mavumbi yao,

   Waipeleka Roho yako,wanaumbwa,nawe waufanya upya uso wa nchi.

3.Utukufu wa Bwana na udumu milele,Bwana na uyafurahie matendo yake.Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake,Mimi nitamfurahia Bwana.

 

Somo la II                              1 Kor. 12: 3-7,12-13

Somo la waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho.

Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Basi pana tofauti za karama, bali Roho ni yeye yule, tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule, Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja  hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristu. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

Neno la Mungu- Tumshukuru Mungu.

 

Aleluya-  Aleluya

Uje Roho Mtakatifu,uzienee nyoyo za waamini wako,

Uwatie mapendo yako      Aleluya aleluya

 

Injili                                                                Yn. 20: 19-23

Somo la Injili takatifu kama iivyoandikwa na Yohana.

Ikawa jioni siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwepo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu,akasimama katikati,akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo,akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomuona Bwana.

Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, Mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.Wowote mtakawaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi,wamefungiwa.

Injili ya Bwana-   Sifa kwako Ee Kristu.

             

Homily

Kipaimara

Sala za Waumini

 

NYIMBO ZA ROHO MTAKATIFU

 

NJOO WANGU MFARIJI

Njoo wangu mfariji, yako shusha mapaji, Roho Mungu njoo

 1. Hekima nishushie na Mungu nimfuate, Roho Mungu njoo.
 2. Akili nijalie, imani nizidishie, Roho Mungu njoo.
 3. Shauri nieleze, nishike njia nzuri, Roho Mungu njoo.
 4. Nguvu nizidishie, nisifanye ulegevu, Roho Mungu njoo.
 5. Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho Mungu njoo.
 6. Ibada niwashie, pekee nikujue, Roho Mungu njoo.
 7. Uchaji nitilie dhambi niichukie, Roho Mungu njoo.

 

NJOO ROHO MTAKATIFU

Njoo roho mtakatifu shusha mapaji (kweli) niwe imara x2

Karibu-karibu (leta) nuru ya mwanga wako ifike moyoni mwangu(leta) x2

1.Roho mwenye hekima roho wa shauri na nguvu.

2.Nipatie elimu nitambue nafsi yako.

3.Nipatie ibada nikusifu daima na milele.

4.Roho mwenye uchaji washa moto wako wa upendo.

 

SHUKA ROHO MUNGU

Shuka Roho wa Mungu njoo kwetu karibu moyoni mwetu, tugawie mapaji yako saba twaomba utuimarishe x2.

1.Shusha mwanga wako na heri zote utujaze neema na upendo uje Baba  wa maskini karibu Baba.

2.Wewe ni rafiki wetu mwema ndiwe mfariji wa Roho zetu, ndiwe nguzo ya imani yetu karibu Baba.

 1. Roho wa elimu na ibada njoo kwetu Baba utuangaze Roho wa hekima na akili karibu Baba.
 2. Tutie nguvu na ujasiri, tudumu katika imani kuu, washa moto wa mapendo karibu Baba.

 

TWAKUOMBA UJE ROHO MFARIJI

1.Twakuomba uje Roho mfariji-uje Roho Mtakatifu mfariji.

Twakuomba uje kutufariji-uje Roho Mtakatifu mfariji.

   Nyoyo zetu ni altare yako, uzipambe kwa mapaji yako uje Roho Mtakatifu mfariji x2

2.Wewe ndiwe Baba mwema na mpaji-uje Roho Mtakatifu mfariji.

Wewe ndiwe mleta kwetu mapaji-uje Roho Mtakatifu mfariji.

3.Utujaze mema yote ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.

Utujaze na faraja ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.

4.Twakuomba uwezo na akili-uje Roho Mtakatifu mfariji.

Twakuomba mapendo yote ya kweli-uje Roho Mtakatifu mfariji.

5.Utuangazie njia ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.

Utuangazie tupate mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.

 

Matoleo          NI SADAKA GANI– M.D.Matonange      Key D

Nitatoa sadaka iliyoje Ee Mungu wangu, ni sadaka gani italingana na wema wako [Kwani kila kitu kinatoka kwako; wewe umeumba vyote nawe ndiwe unayejua hata bila kuombwa, Sasa mimi nikupe nini kikupendeze x2]

1.Kila kitu nilichonacho kimetoka kwako,wewe umenipa mimi  kinifae maishani.

2.Aliyetajiri wa mali nyingi  zimetoka kwako, wewe umempa yeye zimfae maishani.

3.Wapo matajiri na masikini waishi pamoja ili walo matajiri wawafae masikini.

4.Wanyeshea mvua mazao yetu yasitawi vyema,ili tupate chakula kitufae maishani.

 

HAZINA MBINGUNI ;   Dr.Basil Tumaini            Key   D  T/S    2/4

Jiwekeeni hazina yenu, hazina yenu mbinguni [mbinguni] kusiko haribika kitu. x2

Kwa nondo wala kutu wala wevi hawavunji jiwekeeni hazina yenu mbinguni .x2

1.Msijiwekee  hazina duniani nondo na  kutu viharibupo na wevi huvunja na kuiba.

2.Bali jiwekeeni hazina yenu mbinguni kusiko haribika kitu kusiko haribika kitu.

3.Kwa kuwa  hazina yako ilipo ndipo na  moyo wako utakapokuwa ndipo na moyo wako utakapokuwa.

 

TOENI KWA MOYO B.J.Kapumpa    Key G

Toeni kwa moyo sadaka kwa Bwana, kwa maana mkono utoao ndio upokeao,

na katika kutoa ndio kupata zaidi x2

1.Basi toeni  kwa ukarimu, ili upate kuzidishiwa.

2.Toa sadaka iliyo Bora, ili upate kilicho bora.

3.Ukimtolea Mungu mabaki, hakika hautafanikiwa.

 

Offertory procession–  

       CHIWO NE NYASAYE– Dennis Ojwang   Key A    T/S  4/4

Anagolo chiwo mara ni Nyasaye wuon nyakalaga kaw mich wa wakelo- Donge  an agolo duto ma an go mich malong’o gi to wachiwo kata mago mawagole puothe mich malong’o gi towachiwo kata mago mawagole dala ero ero wasongo ero ero wanyoro gisironyo ero ero wakelo mich ma wan go ni Nyasaye nyakalaga.

1.Ngimawa en emorito kindawa enemojiwo tijewa enemokonyo wagol ne uru sadaka

kawuono mondo wayudi hawi.

2.En emaorito dala, en emaogwedho dala en emaokonyo dala… wagol ne uru sadaka

kawuono mondo….

3.Kata rieko ma wang’ado kata kinda ka watimo kata chiwo wa magolo- wagol ne uru

sadaka….

4.En emoyawo nwa yo, en emogeng’o touché en emokelo ngima-wagol ne uru sadaka

kawuono mondo..

 

Chetezo–           Ee Bwana  IkupendezeJoseph D. Nkomagu    Key   G   T/S  3/8

Ee Bwana ikupendeze, Bwana ikupendeze,sadaka ya sikukuu hii ya leo x2

Sadaka hii ndiyo fidia timilifu, ya kutupatanisha na wewe Mungu Baba,

 na pia Ibada timilifu, ya kukutolea wewe Ee Mungu wetu.             

1.Tunakutolea Mkate na divai,  kazi ya mikono yetu  wanadamu twakuomba  Ee Baba uvipokee.

2.Tunakutolea pia na fedha zetu, pia na mazao  ya mashamba yetu, twakuomba  Ee Baba uyapokee.

3.Tunakutolea nazo nafsi zetu, kwa unyenyekevu  na kwa moyo safi, twakuomba  Ee Baba uzipokee.

 

MTAKATIFUMillenium MassJohn Mwendwa

Mtakatifu Bwana Mtakatifu Bwana mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi  x2
Mbingu na dunia mbingu na dunia zimejaa kweli utukufu wako X 2

Hosana juu hosanna juu hosanna juu mbinguni x 2

Mbarikiwa yule mbarikiwa yule yule mwenye kuja kwa jina la Bwana x2

 

FUMBO LA IMANIFadhili Mass Key A

Ee Bwana, tunatangaza kifo chako-Na kutukuza ufufuko wako Mpaka utakapokuja.

 

Amina- Subukia shrine Mass    Key G

Amina amina, amina amina  x2

 

BABA YETU     reciting

 

Amani-

1.Tupe Amani,Bwana tupe amani,tupe amani Bwana tupe amanix2

Wololowololo amani,amani,amani,amani x2

2.Tupe Upendo          3.Tupe Faraja            4.Tupe Fadhili

 

MWANAKONDOO – Millenium Mass  Key G

Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utuhurumie

Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utuhurumie

Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utujalie Amani

 

Komunio- KARIBUNI KWA KARAMU- Ernest Mwasaru  Key G

Karibuni kwa karamu ni karamu takatifu twende twende tumpokee x2

twende twendeni tumealikwa twende twende tumpokee x2

1.Ni mwili na damuye,Yesu Mwana wa Mungu twende twende kwa karamu

2.Yesu anatulisha chakula cha mbinguni..

3.Anatupa uzima na kutuimarisha..

4.Twendeni kwa imani tumpokee mwokozi..

5.Yesu ndiye mkate utokao mbinguni..

 

TUJONGEE MEZANI Meriack Kavakule  Key D

Tujongee mezani mezani  kwa Bwana, x2 [ili] tukauonje utamu mbingu x2

1.Mwili wake Bwana Yesu ni chakula,damu yake Bwana Yesu kinywaji safi.

2.Aulaye mwili wake ana uzima, ainywaye damu yake taburudishwa.

3.Hima hima twende wote tukampokee,ili tupate uzima war oho zetu.

4.Ukarimu wake Bwana wa ajabu, kwani ametuandalia mezani pake.

     

TUKAMPOKEE YESU  Tumaini Swai   Key  Ab

Karamu yake Bwana Yesu kweli imekwisha  kuandaliwa tujongee wote wenye moyo safi tukampokee x2 Twendeni kwenye meza ya upendo tukale mwili wake Bwana Yesu tukanywe damu yake Bwana Yesu Yeye ndiye  chemchemi ya uzima war oho zetu uzima ule wa milele x2

01.Mwili  wa Yesu  ni chakula kweli, kilicho shuka toka mbinguni kwa ajili ya roho zetu

twendeni haya twendeni tukampokee.

2.Damu ya Yesu  ni kinywaji kweli  kilichoshuka kutoka mbinguni kwa ajili ya roho zetu

twendeni…

 1. Tulapo mwili na kunywa damuyake Yesu tunatangaza kifo chake na kutukuza ufufuko wake

twendeni..        

 

Kushukuru           ASANTE YESU KATIKA EKARISTI- F.Kashumba    Key D

Asante Yesu kutulisha mwili wako, Asante Yesu kutunywesha damu yako,

Umetulisha kwa mwili umetunywesha kwa damu, Asante Yesu katika Ekaristi x2.

1.Umetulisha, umetunywesha, Asante Yesu, asante Yesu.

2.Utushibishe kwa mwili wako, Ututakase kwa damu yako.

3.Mwili wa Kristu, uniokoe, Damu ya Kristu nifurahishe.

4.Roho ya Kristu, initakase, asante Yesu wa Ekaristi.

 

NAOMBA BARAKA– J.M.Salisali  Key E, T/S 3/8

Kama ulivyo wingi wa nyota  za angani ninaomba Bwana uyajaza Baraka maisha yangu x2

[Neema zinitiririkie, rehema zinitiririkie, naomba furaha yako bwana, naomba faraja yako Bwana, ninaomba Bwana uyajaza Baraka maisha yangu x2]

1.Kama ile Baraka uliyomjalia/ Baba yetu mtumishi wako Abrahamu/

Mfano wa nyota za angani mithili ya mchanga wa pwani ninaomba nijalie na mimi Baraka.

2.Na kama Yakobo na uzao wake wote/ Baraka uliujaza kwa upendo/

Maana wewe una uwezo na nguvu asili ya vyote naomba nijalie  na mimi Baraka.

3.Unijaze nguvu na akili ki-imani/ Nahitaji mwanga na mwongozo wako Mungu

Daima uwe name Ee Bwana milele nikufuate wewe naomba nijalie  na mimi Baraka

 

Mwisho–           TWAKUSALIMU MAMA MARIA– Sr.Alice Sambu    Key G       T/S  4/4

 Twakusalimu Mama Maria  Mama wa Kristu utuombee x2

1.Mama wa Muumba utuombee, Mama wa mkombozi utuombee x2

2.Bikira wa huruma utuombeeBikira mwaminifu utuombee x2

3.Kioo cha haki utuombee kikao cha hekima utuombee x2

4.Chombo cha neema  utuombee chombo cha ibada utuombee x2

5.Mnara wa Daudi utuombee mnara wa pembe  utuombee

6.Afya ya wagonjwa utuombee msaada wa wakristu-utuombee x2

7.Malkia wa manabii utuombee, Malkia wa mitume utuombee

8.Malkia wa Rosari utuombee, Malkia wa amani utuombee x2

 

 

MARIA  UNAPENDEZA   Merriack Kavakule        Key  G

Mama Maria kwa hakika unapendeza, jina lako  ni tamu sana kutamka x2

Nilitajapo jina Maria  ninafarijika moyoni mwangu x2

1.Wewe mwombezi wetu Mama yetu Maria, salamu tunakusalimu Maria.

2.Pokea shangwe zetu tunakushangilia, salamu tunakusalimu Maria.

3.Wewe Mama Maria ndiwe Mama yetu, salamu tunakusalimu Maria

4.Nasi tunajivuna kutaja jina lako, salamu tunakusalimu Maria.

 

SIMAMA IMARA [DO NOT BE AFRAID]

Simama imara katika Imani x2 usiogope, usiogope, usiogope tulia katika maombi,]

[Do not be afraid, do not be afraid, do not be afraidStand strong in faith.

1.Watesi wako wanapokuzunguka, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule

2.Hata shetani abishe kwako  mpenzi, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule

3.Uwapo kwenye giza totoro, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule

 

NITAMSIFU MUNGU   Key G

Nitamsifu Mungu wa mbinguni aliyeniumba

Ananipenda tena anilinda kati ya mabaya x 2

1.Alinipenda –Kuliko vyote –Akaniumba –Kwa mfano wake –

Uhai wangu –Najivunia –Kwani najua anipenda

 1. Viungo vyote –Vya mwili wangu –Vyamtukuza –Vyamuabudu –

Najitolea –Maisha yangu –Kufanya kazi yake Bwana

 1. Ninakuomba –Unipe nguvu –Yakukusifu –Na kukupenda –

Siku kwa siku –Nikutukuze –Kwani wewe ni Mungu wangu

 

BWANA UNIFANYE NIWE CHOMBO Key  G

Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako x 2

1.Palipo na chuki nilete amani, amani yako, palipo ugomvi nilete msamaha wako

 1. Palipo na shida nilete tumaini, tumaini lako palipo na giza nilete mwangaza Bwana
 2. Palipo uchungu nilete furaha, furaha yako , Bwana nijalie niwe chombo cha kufaa.

 

Uninyunyizie maji

Uninyunyizie maji Bwana uninyunyizie maji Bwana unioshe nitakate

[mimi]niwe mweupe kabisa x2

1.Natamani nije kwako-Bwana x2                           2.Naingia nyumba yako-Bwana x2

3.Niuone uso wako-Bwanax2                                  4.Nifurahi milele-Bwana

 

NINAKUPENDA MUNGU-Victor Murishiwa

Ninakupenda Mungu (wangu) ninakupenda wewe milele na milele (bwana) nitakutukuza, pokea sifa zangu (bwana) zinazotoka katika kinywa changu  mimi (ndani) na moyoni mwamgu x2.

1.Katika makusanyiko, nitaziimba zaburi, nitazitangaza sifa, zake

daima milele, kwenye madhabahu yako, nitaitoa sadaka ile ya

kukupendeza, ee Baba muumba wangu.

2.Umenitendea mengi, mema yasio idadi, ninakushukuru Baba,

muumba wa ulimwengu, nikiyakumbuka yote machozi

yanimwagika, ni machozi ya furaha ni machozi ya upendo.

3.Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe ukinitupa wewe, nani

ataniokota, Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii, dunia yenye

mateso, na yenye mahangaiko.

 

MAJI YA KIPEKEE Emmanuel Kiti    Key C

1.Ndiyo maji mema kweli toka kwa Bwana-tukanyunyiziweni tupate uzima x2

Njoni kina baba njoni kina mama nanyi enyi watoto tupate uzima x2

2.maji yenye uvivio wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2

3.Maji yenye ubaridi wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2

4.Ni maji yenye barakaza kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2

5.Maji yenye utakaso wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2

6.Ni maji kweli ya Roho Mtakatifu- tukanyunyiziweni tupate uzima x2

 

SALA KWA AJILI YA SINODI

Tunasimama mbele yako Ewe Roho Mtakatifu, tunapokusanyika pamoja kwa jina lako,

Wewe pekee unayetuongoza, weka maskani yako ndani ya nyoyo yetu, utufundishe njia ya kupita na jinsi ya kuenenda. Sisi ni dhaifu na wenye dhambi, Usiruhusu tuendelee kuchochea machafuko, Usiruhusu ujinga utuongoze kwenye  njia mbaya wala utepetevu usiadhiri matendo yetu. Utuwezeshe ndani yako tuwe na umoja, Ili tuweze kusafiri pamoja hadi uzima wa milele, wala tusipotee mbali kutoka njia ya kweli na iliyo sahihi. Tunaomba hayo yote, kwako wewe ufanyaye  kazi kila mahali na kila wakati, katika ushirika wa Baba na Mwana, milele na milele, Amina

 

Details

Date:
May 18
Event Category: