- This event has passed.
GOLDEN JUBILEE CELEBRATONS (Parokia ya Kikambala 18Th May 2024)
May 18
PROGRAM
0900 : Arrival of invited Guests
10.00 : Start of Holy Mass
Entrance Hymn & opening Prayer
Pentential Rites & Gloria
Readings- Somo la 1-
Wimbo wa Katikati
Somo la 2-
Injili
Kipaimara
Sala za waumini-
Sadaka
Sala ya Ekaristi
Komunio
Sala baada ya Komunio
Wimbo wa Shukurani
matangazo
1200: Baraka na Wimbo wa Mwisho
Nyimbo za Misa
Mwanzo-
TWENDENI KWAKE MUNGU By Mwahunga James Munga Key G
Twendeni kwake Mungu (Twendeni kwa Mungu),
kwa shangwe na ndereme (Shangwe na nderemo);
Kwa kinanda na nyimbo tukamwabudu, na kayamba na ngoma tukamwabudu x 2
- Nyumbani mwa Mungu tuingie kwa shangwe, kwa nyimbo za sifa tumwabuda.
- Ni Mungu muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyomo.
- Na kila mwenye pumzi amsifu Mungu, na kila kiumbe kimsujudie.
- Aliyetuumba anatupenda, aliyetukomboa atupenda.
- Ni kwa upendo wake twajazwa neema, kwa wema wake twasamehewa.
Kumekucha – B.Mukasa Key G
1.Kumekucha-ni sikukuu ya ajabu leo hii x2
Watu wote-wanameremeta tazama,
Wamevaa-mavazi mazuri oneni
Nyuso zao-tabasamu shangwe nderemo na vifijo
2.Twimbe wote-ni sikukuu ya ajabu leo hii
Tufurai-….
3.Mungu wetu…………..Katukuka………
4.Katupenda…………….Katuinua…………
5.Pendo gani………….Ametupa……..
6.Raha tele……………Mustarehe………..
NJOONI TUINGIE Key G David Okoth Onyango
1.Njooni tuingie nyumbani mwa Bwana-Njooni tuingie nyumani mwake
Wazee ingieni nyumbani mwa Bwana-Njooni tuingie nyumbani mwake
Tunaingia-kwa vifijo na shangwe, Kwa ngoma safi- na madaha na maringo
Tujiandae-tuombe radhi kwa Mungu Atutakase-tukamtolee sadaka.
2.Vijana furahieni ulinzi wa Mungu-njooni tumshukuru Mungu wetu
Pamoja tujongee tupige makofi-njooni tumshukuru mlinzi wetu
3.Mwenyezi atupenda kwa pendo la kweli-njooni tumsujudu Muumba wetu
Kwa kweli tumeumbwa kwa mfano wake-njooni tumsujudu muumba wetu
Chetezo BWANA AMENITUMA Bruno S.Mpepo Key A
Bwana amenituma kuwahubiri mataifa, Bwana amenituma mimi x2
Bwana amenitia mafuta kuhubiri habari njema x2
1.Roho wa Bwana yu juu yangu,kwa maana amenipaka mafuta,kuwahubiri masikini habari njema.
2.Amenituma kutangaza kufunguliwa kwao wafungwa nao vipofu kupata kuona tena
3.Kuponywa waliovunjika moyo kuwafariji wote waliao kuwapatia maua badala ya jivu
BWANA : MISA MILLENIUM -Key G John Mwendwa
Bwana Bwana Bwana utuhurumie x2
Kristu Kristu [Kristu] utuhurumie x2
Bwana Bwana Bwana utuhurumie x2
UTUKUFU :
1.Utukufu kwa Mungu juu mbinguni Na amani duniani-Kwa watu aliowaridhia
Tunakusifu,tunakuheshimu,tunakuabudu,tunakutukuza
2.Tunakushukuru kwa ajili, Ya utukufu wako mkuu- Ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni
- Mungu Baba Baba mwenyezi, Ee Bwana Yesu Kristu Mwana pekee Ee Bwana Mungu.
4.Mwanakondoo wa Mungu Mwana wa Baba, Mwenye kuondoa dhambi, za ulimwengu utuhurumie.
5.Mwenye kuondoa dhambi, dhambi za ulimwengu, pokea ombi letu
- Mwenye kuketi kuume kwa Baba. Utuhurumie kwa kuwa ndiwe, uliye pekee yako mtakatifu
7.Pekee yako Bwana pekee yako, uliye juu kabisa Yesu,Yesu Kristu.
- Pamoja na-Roho mtakatifu, katika utukufu, wa Mungu Baba Amina.
Bible Procession-
UZURI WA YESU Alfred Ossonga Key C T/S 2/4
Kwa imani yangu matendo na maneno, nihubiri neno la Mungu siku zote,
Nipeleke neno la Mungu pande zote, mataifa wanangojea neno hilo x 2
1.Kwa ajili yake Yesu Kristo Bwana wangu, kwa ajili ya uzuri wake wa Daima,
Uzuri wake Yesu usio na kiasi, nitende yote mema nifanane na Yesu
- Kwa ajili yake Yesu Kristo Bwana wangu, nimeyasahau maneno ya zamani,
Ya kale yamepita shetani ameshindwa, nimempata Yesu natembea na yeye
3.Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu, Kwa ajili ya uzuri wake wa daima,
nakaza mwendo sana nipeleke ujumbe, ujumbe wake Yesu kwa amataifa yote.
Somo la 1. Mdo: 2, 1-11
Somo Kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume.
Ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi. Ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za motouliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kusema kwa lugha , kama Roho alivyowajalia kutamka.
Na kulikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Waparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapedokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia,Misri na pande za Libia karibu na Kirene , na wageni watokao Rumi. Wayahudi na Waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
Neno la Mungu- Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa katikati Zab. 104; 1,24,29-31, 34. K-30
Waipeleka Roho yako-Venas Lujinya Key D
Waipeleka Roho yako, Ee Bwana Ee Bwana,
nawe waufanya upya uso wa nchi-Aleluya
1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,Wewe Bwana Mungu wangu, umejifanya mkuu sana
Ee Bwana jinsi yalivyo mengi matendo yako,Dunia imejaa mali zako.
2.Waiondoa pumzi yao wanakufa na kuyarudia mavumbi yao,
Waipeleka Roho yako,wanaumbwa,nawe waufanya upya uso wa nchi.
3.Utukufu wa Bwana na udumu milele,Bwana na uyafurahie matendo yake.Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake,Mimi nitamfurahia Bwana.
Somo la II 1 Kor. 12: 3-7,12-13
Somo la waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho.
Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. Basi pana tofauti za karama, bali Roho ni yeye yule, tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule, Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristu. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
Neno la Mungu- Tumshukuru Mungu.
Aleluya- Aleluya
Uje Roho Mtakatifu,uzienee nyoyo za waamini wako,
Uwatie mapendo yako Aleluya aleluya
Injili Yn. 20: 19-23
Somo la Injili takatifu kama iivyoandikwa na Yohana.
Ikawa jioni siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwepo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu,akasimama katikati,akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo,akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomuona Bwana.
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, Mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.Wowote mtakawaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi,wamefungiwa.
Injili ya Bwana- Sifa kwako Ee Kristu.
Homily
Kipaimara
Sala za Waumini
NYIMBO ZA ROHO MTAKATIFU
NJOO WANGU MFARIJI
Njoo wangu mfariji, yako shusha mapaji, Roho Mungu njoo
- Hekima nishushie na Mungu nimfuate, Roho Mungu njoo.
- Akili nijalie, imani nizidishie, Roho Mungu njoo.
- Shauri nieleze, nishike njia nzuri, Roho Mungu njoo.
- Nguvu nizidishie, nisifanye ulegevu, Roho Mungu njoo.
- Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho Mungu njoo.
- Ibada niwashie, pekee nikujue, Roho Mungu njoo.
- Uchaji nitilie dhambi niichukie, Roho Mungu njoo.
NJOO ROHO MTAKATIFU
Njoo roho mtakatifu shusha mapaji (kweli) niwe imara x2
Karibu-karibu (leta) nuru ya mwanga wako ifike moyoni mwangu(leta) x2
1.Roho mwenye hekima roho wa shauri na nguvu.
2.Nipatie elimu nitambue nafsi yako.
3.Nipatie ibada nikusifu daima na milele.
4.Roho mwenye uchaji washa moto wako wa upendo.
SHUKA ROHO MUNGU
Shuka Roho wa Mungu njoo kwetu karibu moyoni mwetu, tugawie mapaji yako saba twaomba utuimarishe x2.
1.Shusha mwanga wako na heri zote utujaze neema na upendo uje Baba wa maskini karibu Baba.
2.Wewe ni rafiki wetu mwema ndiwe mfariji wa Roho zetu, ndiwe nguzo ya imani yetu karibu Baba.
- Roho wa elimu na ibada njoo kwetu Baba utuangaze Roho wa hekima na akili karibu Baba.
- Tutie nguvu na ujasiri, tudumu katika imani kuu, washa moto wa mapendo karibu Baba.
TWAKUOMBA UJE ROHO MFARIJI
1.Twakuomba uje Roho mfariji-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Twakuomba uje kutufariji-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Nyoyo zetu ni altare yako, uzipambe kwa mapaji yako uje Roho Mtakatifu mfariji x2
2.Wewe ndiwe Baba mwema na mpaji-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Wewe ndiwe mleta kwetu mapaji-uje Roho Mtakatifu mfariji.
3.Utujaze mema yote ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Utujaze na faraja ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.
4.Twakuomba uwezo na akili-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Twakuomba mapendo yote ya kweli-uje Roho Mtakatifu mfariji.
5.Utuangazie njia ya mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Utuangazie tupate mbingu-uje Roho Mtakatifu mfariji.
Matoleo NI SADAKA GANI– M.D.Matonange Key D
Nitatoa sadaka iliyoje Ee Mungu wangu, ni sadaka gani italingana na wema wako [Kwani kila kitu kinatoka kwako; wewe umeumba vyote nawe ndiwe unayejua hata bila kuombwa, Sasa mimi nikupe nini kikupendeze x2]
1.Kila kitu nilichonacho kimetoka kwako,wewe umenipa mimi kinifae maishani.
2.Aliyetajiri wa mali nyingi zimetoka kwako, wewe umempa yeye zimfae maishani.
3.Wapo matajiri na masikini waishi pamoja ili walo matajiri wawafae masikini.
4.Wanyeshea mvua mazao yetu yasitawi vyema,ili tupate chakula kitufae maishani.
HAZINA MBINGUNI ; Dr.Basil Tumaini Key D T/S 2/4
Jiwekeeni hazina yenu, hazina yenu mbinguni [mbinguni] kusiko haribika kitu. x2
Kwa nondo wala kutu wala wevi hawavunji jiwekeeni hazina yenu mbinguni .x2
1.Msijiwekee hazina duniani nondo na kutu viharibupo na wevi huvunja na kuiba.
2.Bali jiwekeeni hazina yenu mbinguni kusiko haribika kitu kusiko haribika kitu.
3.Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo na moyo wako utakapokuwa ndipo na moyo wako utakapokuwa.
TOENI KWA MOYO– B.J.Kapumpa Key G
Toeni kwa moyo sadaka kwa Bwana, kwa maana mkono utoao ndio upokeao,
na katika kutoa ndio kupata zaidi x2
1.Basi toeni kwa ukarimu, ili upate kuzidishiwa.
2.Toa sadaka iliyo Bora, ili upate kilicho bora.
3.Ukimtolea Mungu mabaki, hakika hautafanikiwa.
Offertory procession–
CHIWO NE NYASAYE– Dennis Ojwang Key A T/S 4/4
Anagolo chiwo mara ni Nyasaye wuon nyakalaga kaw mich wa wakelo- Donge an agolo duto ma an go mich malong’o gi to wachiwo kata mago mawagole puothe mich malong’o gi towachiwo kata mago mawagole dala ero ero wasongo ero ero wanyoro gisironyo ero ero wakelo mich ma wan go ni Nyasaye nyakalaga.
1.Ngimawa en emorito kindawa enemojiwo tijewa enemokonyo wagol ne uru sadaka
kawuono mondo wayudi hawi.
2.En emaorito dala, en emaogwedho dala en emaokonyo dala… wagol ne uru sadaka
kawuono mondo….
3.Kata rieko ma wang’ado kata kinda ka watimo kata chiwo wa magolo- wagol ne uru
sadaka….
4.En emoyawo nwa yo, en emogeng’o touché en emokelo ngima-wagol ne uru sadaka
kawuono mondo..
Chetezo– Ee Bwana Ikupendeze– Joseph D. Nkomagu Key G T/S 3/8
Ee Bwana ikupendeze, Bwana ikupendeze,sadaka ya sikukuu hii ya leo x2
Sadaka hii ndiyo fidia timilifu, ya kutupatanisha na wewe Mungu Baba,
na pia Ibada timilifu, ya kukutolea wewe Ee Mungu wetu.
1.Tunakutolea Mkate na divai, kazi ya mikono yetu wanadamu twakuomba Ee Baba uvipokee.
2.Tunakutolea pia na fedha zetu, pia na mazao ya mashamba yetu, twakuomba Ee Baba uyapokee.
3.Tunakutolea nazo nafsi zetu, kwa unyenyekevu na kwa moyo safi, twakuomba Ee Baba uzipokee.
MTAKATIFU –Millenium Mass–John Mwendwa
Mtakatifu Bwana Mtakatifu Bwana mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi x2
Mbingu na dunia mbingu na dunia zimejaa kweli utukufu wako X 2
Hosana juu hosanna juu hosanna juu mbinguni x 2
Mbarikiwa yule mbarikiwa yule yule mwenye kuja kwa jina la Bwana x2
FUMBO LA IMANI –Fadhili Mass Key A
Ee Bwana, tunatangaza kifo chako-Na kutukuza ufufuko wako Mpaka utakapokuja.
Amina- Subukia shrine Mass Key G
Amina amina, amina amina x2
BABA YETU reciting
Amani-
1.Tupe Amani,Bwana tupe amani,tupe amani Bwana tupe amanix2
Wololowololo amani,amani,amani,amani x2
2.Tupe Upendo 3.Tupe Faraja 4.Tupe Fadhili
MWANAKONDOO – Millenium Mass Key G
Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu – uondoaye dhambi za ulimwengu utujalie Amani
Komunio- KARIBUNI KWA KARAMU- Ernest Mwasaru Key G
Karibuni kwa karamu ni karamu takatifu twende twende tumpokee x2
twende twendeni tumealikwa twende twende tumpokee x2
1.Ni mwili na damuye,Yesu Mwana wa Mungu twende twende kwa karamu
2.Yesu anatulisha chakula cha mbinguni..
3.Anatupa uzima na kutuimarisha..
4.Twendeni kwa imani tumpokee mwokozi..
5.Yesu ndiye mkate utokao mbinguni..
TUJONGEE MEZANI Meriack Kavakule Key D
Tujongee mezani mezani kwa Bwana, x2 [ili] tukauonje utamu mbingu x2
1.Mwili wake Bwana Yesu ni chakula,damu yake Bwana Yesu kinywaji safi.
2.Aulaye mwili wake ana uzima, ainywaye damu yake taburudishwa.
3.Hima hima twende wote tukampokee,ili tupate uzima war oho zetu.
4.Ukarimu wake Bwana wa ajabu, kwani ametuandalia mezani pake.
TUKAMPOKEE YESU Tumaini Swai Key Ab
Karamu yake Bwana Yesu kweli imekwisha kuandaliwa tujongee wote wenye moyo safi tukampokee x2 Twendeni kwenye meza ya upendo tukale mwili wake Bwana Yesu tukanywe damu yake Bwana Yesu Yeye ndiye chemchemi ya uzima war oho zetu uzima ule wa milele x2
01.Mwili wa Yesu ni chakula kweli, kilicho shuka toka mbinguni kwa ajili ya roho zetu
twendeni haya twendeni tukampokee.
2.Damu ya Yesu ni kinywaji kweli kilichoshuka kutoka mbinguni kwa ajili ya roho zetu
twendeni…
- Tulapo mwili na kunywa damuyake Yesu tunatangaza kifo chake na kutukuza ufufuko wake
twendeni..
Kushukuru ASANTE YESU KATIKA EKARISTI- F.Kashumba Key D
Asante Yesu kutulisha mwili wako, Asante Yesu kutunywesha damu yako,
Umetulisha kwa mwili umetunywesha kwa damu, Asante Yesu katika Ekaristi x2.
1.Umetulisha, umetunywesha, Asante Yesu, asante Yesu.
2.Utushibishe kwa mwili wako, Ututakase kwa damu yako.
3.Mwili wa Kristu, uniokoe, Damu ya Kristu nifurahishe.
4.Roho ya Kristu, initakase, asante Yesu wa Ekaristi.
NAOMBA BARAKA– J.M.Salisali Key E, T/S 3/8
Kama ulivyo wingi wa nyota za angani ninaomba Bwana uyajaza Baraka maisha yangu x2
[Neema zinitiririkie, rehema zinitiririkie, naomba furaha yako bwana, naomba faraja yako Bwana, ninaomba Bwana uyajaza Baraka maisha yangu x2]
1.Kama ile Baraka uliyomjalia/ Baba yetu mtumishi wako Abrahamu/
Mfano wa nyota za angani mithili ya mchanga wa pwani ninaomba nijalie na mimi Baraka.
2.Na kama Yakobo na uzao wake wote/ Baraka uliujaza kwa upendo/
Maana wewe una uwezo na nguvu asili ya vyote naomba nijalie na mimi Baraka.
3.Unijaze nguvu na akili ki-imani/ Nahitaji mwanga na mwongozo wako Mungu
Daima uwe name Ee Bwana milele nikufuate wewe naomba nijalie na mimi Baraka
Mwisho– TWAKUSALIMU MAMA MARIA– Sr.Alice Sambu Key G T/S 4/4
Twakusalimu Mama Maria Mama wa Kristu utuombee x2
1.Mama wa Muumba utuombee, Mama wa mkombozi utuombee x2
2.Bikira wa huruma utuombeeBikira mwaminifu utuombee x2
3.Kioo cha haki utuombee kikao cha hekima utuombee x2
4.Chombo cha neema utuombee chombo cha ibada utuombee x2
5.Mnara wa Daudi utuombee mnara wa pembe utuombee
6.Afya ya wagonjwa utuombee msaada wa wakristu-utuombee x2
7.Malkia wa manabii utuombee, Malkia wa mitume utuombee
8.Malkia wa Rosari utuombee, Malkia wa amani utuombee x2
MARIA UNAPENDEZA Merriack Kavakule Key G
Mama Maria kwa hakika unapendeza, jina lako ni tamu sana kutamka x2
Nilitajapo jina Maria ninafarijika moyoni mwangu x2
1.Wewe mwombezi wetu Mama yetu Maria, salamu tunakusalimu Maria.
2.Pokea shangwe zetu tunakushangilia, salamu tunakusalimu Maria.
3.Wewe Mama Maria ndiwe Mama yetu, salamu tunakusalimu Maria
4.Nasi tunajivuna kutaja jina lako, salamu tunakusalimu Maria.
SIMAMA IMARA [DO NOT BE AFRAID]
Simama imara katika Imani x2 usiogope, usiogope, usiogope tulia katika maombi,]
[Do not be afraid, do not be afraid, do not be afraidStand strong in faith.
1.Watesi wako wanapokuzunguka, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule
2.Hata shetani abishe kwako mpenzi, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule
3.Uwapo kwenye giza totoro, Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwenyezi Mungu ewe mteule
NITAMSIFU MUNGU Key G
Nitamsifu Mungu wa mbinguni aliyeniumba
Ananipenda tena anilinda kati ya mabaya x 2
1.Alinipenda –Kuliko vyote –Akaniumba –Kwa mfano wake –
Uhai wangu –Najivunia –Kwani najua anipenda
- Viungo vyote –Vya mwili wangu –Vyamtukuza –Vyamuabudu –
Najitolea –Maisha yangu –Kufanya kazi yake Bwana
- Ninakuomba –Unipe nguvu –Yakukusifu –Na kukupenda –
Siku kwa siku –Nikutukuze –Kwani wewe ni Mungu wangu
BWANA UNIFANYE NIWE CHOMBO Key G
Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako x 2
1.Palipo na chuki nilete amani, amani yako, palipo ugomvi nilete msamaha wako
- Palipo na shida nilete tumaini, tumaini lako palipo na giza nilete mwangaza Bwana
- Palipo uchungu nilete furaha, furaha yako , Bwana nijalie niwe chombo cha kufaa.
Uninyunyizie maji
Uninyunyizie maji Bwana uninyunyizie maji Bwana unioshe nitakate
[mimi]niwe mweupe kabisa x2
1.Natamani nije kwako-Bwana x2 2.Naingia nyumba yako-Bwana x2
3.Niuone uso wako-Bwanax2 4.Nifurahi milele-Bwana
NINAKUPENDA MUNGU-Victor Murishiwa
Ninakupenda Mungu (wangu) ninakupenda wewe milele na milele (bwana) nitakutukuza, pokea sifa zangu (bwana) zinazotoka katika kinywa changu mimi (ndani) na moyoni mwamgu x2.
1.Katika makusanyiko, nitaziimba zaburi, nitazitangaza sifa, zake
daima milele, kwenye madhabahu yako, nitaitoa sadaka ile ya
kukupendeza, ee Baba muumba wangu.
2.Umenitendea mengi, mema yasio idadi, ninakushukuru Baba,
muumba wa ulimwengu, nikiyakumbuka yote machozi
yanimwagika, ni machozi ya furaha ni machozi ya upendo.
3.Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe ukinitupa wewe, nani
ataniokota, Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii, dunia yenye
mateso, na yenye mahangaiko.
MAJI YA KIPEKEE Emmanuel Kiti Key C
1.Ndiyo maji mema kweli toka kwa Bwana-tukanyunyiziweni tupate uzima x2
Njoni kina baba njoni kina mama nanyi enyi watoto tupate uzima x2
2.maji yenye uvivio wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2
3.Maji yenye ubaridi wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2
4.Ni maji yenye barakaza kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2
5.Maji yenye utakaso wa kipekee- tukanyunyiziweni tupate uzima x2
6.Ni maji kweli ya Roho Mtakatifu- tukanyunyiziweni tupate uzima x2
SALA KWA AJILI YA SINODI
Tunasimama mbele yako Ewe Roho Mtakatifu, tunapokusanyika pamoja kwa jina lako,
Wewe pekee unayetuongoza, weka maskani yako ndani ya nyoyo yetu, utufundishe njia ya kupita na jinsi ya kuenenda. Sisi ni dhaifu na wenye dhambi, Usiruhusu tuendelee kuchochea machafuko, Usiruhusu ujinga utuongoze kwenye njia mbaya wala utepetevu usiadhiri matendo yetu. Utuwezeshe ndani yako tuwe na umoja, Ili tuweze kusafiri pamoja hadi uzima wa milele, wala tusipotee mbali kutoka njia ya kweli na iliyo sahihi. Tunaomba hayo yote, kwako wewe ufanyaye kazi kila mahali na kila wakati, katika ushirika wa Baba na Mwana, milele na milele, Amina