Skip to content Skip to footer
Loading Events

« All Events

  • This event has passed.

Solemn Profession Program

August 17 @ 9:30 AM - 5:00 PM

Program

  • Beginning of Mass 3
  • Liturgy of the Word 5
  • Rite of Profession 7
  •  Liturgy of the Eucharist 11
  •  Speeches and Announcement
    • Chair Moderator
    • Representative of Parents
    • Representative of the newly professed Brothers
    • Parish Priest
    • Provincial
  • Final Blessing

1. ENTRANCE SONGS

NJOONI TUMFANYIE SHANGWE

SOP: Njooni tumfanyie shangwe
Mungu wetu-Njooni…
SOP: Jongeeni nyote tuimbe kwa
pamoja- Njooni…
Ten: Kwa miondoko ya raha na
kucheza- Njooni…
Bass: Kwa ngoma safi, tamu na
midundiko- Njooni…
Tumpigie-makofi makofi makofi
(makofi)
SOP: Bwana ametenda mambo ya
ajabu- Njooni…
SOP: Machozi ameyageuza kichekonjooni…
TEN: Tumuimbie leo tumsifu yeyenjooni…
BASS: Tukipigapiga vifua kwa
maringo-njooni…
Tumpigie-makofi makofi makofi
(makofi)
umpokeeni Bwana kwa madaa-njooni…
Ajue kwamba leo tumefurahi njooni…
Na shingo zinesenese kwa vinundonjooni…
Mwili uyumbeyumbe kushoto kulia
–njooni…
Tumpigie-makofi makofi makofi
(makofi)
Watoto nao wabebwe juu juunjooni….
Wajue kwamba Mungu anawapendanjooni…

Umati wote turukeruke juunjooni Tusisitesite Mungu yu kati yetu
njooni…
Tumpigie-makofi makofi makofi
(makofi)

NALIFURAHI SANA
(John Matoke)

Nalifurahi sana waliponiambia
-na twende,
furahi sana waliponiambia-na twende,
(nyumbani mwa Baba twende.)x2
1. Nitakushukuru kwa moyo wangu
wote –
nitakushukuru
Mbele ya miungu kuimba zaburi –
Nalifurahi sana waliponiambia
-na twende,
furahi sana waliponiambia- na
twende,
(nyumbani mwa Baba twende.)x2
2. Nitakusujudu katika nyumba yako –
nitakushukuru
Nitalishukuru jina lako ee bwanaNalifurahi sana waliponiambia
-na twende,
furahi sana waliponiambia- na
twende,
(nyumbani mwa Baba twende.)x2
3. Kwa fadhili zako na uaminifu wakonitakushukuru
Kwa maana wewe umekuza ahadiNalifurahi sana waliponiambia
-na twende,
furahi sana waliponiambia- na
twende,
(nyumbani mwa Baba twende.)x2

4. Nilipokuita uliniitikianitakushukuru
Ukanifariji ukanitia nguvuNalifurahi sana waliponiambia
-na twende,
furahi sana waliponiambia- na
twende,
(nyumbani mwa Baba twende.)x2

OUR LADY OF MERCY MASS

1. Bwana tuhurumie, Bwana
tuhurumie, (Bwana tuhurumie,
sisi wakosefu.) ×2
2. Kristu tuhurumie, Kristu
tuhurumie, (Kristu tuhurumie,
sisi wakosefu.) ×2
3. Bwana tuhurumie, Bwana
tuhurumie, (Bwana tuhurumie,
sisi wakosefu.) ×2

(UTUKUFU)

Ten: Utukufu kwa Mungu mbinguni.
CHORUS: (Utukufu kwa Mungu
mbinguni, na amani duniani, kwa
watu waatu, kwa watu wenye
mapenzi mema.) x2
1. Tunakusifu twaheshimu,
twakuabudu twakutukuza;
twakushukuru mfalme wa mbingu,
Mwana wa pekee, Mwana wa Baba.
–Bwana.
2. Unayeondoa makosa yetu,
tuhurumie tusikilize;
Kuume kwa Baba unapoketi,
Mtakatifu mkuu tuhurumie.
–Bwana.

3. Pamoja na Roho Mtakatifu,
ndani ya Baba unatukuzwa;
Mungu mmoja anayeishi,
ndiye mtawala milele yote.
– Bwana.

INASONGA MBELE INJILI

{Inasonga mbele injili, inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga
mbele.}x2
1. Kwa vijana inasonga inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga
mbele.
Kwa wazee inasonga; inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga mbele.
{Inasonga mbele injili, inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga
mbele.}x2
2. Kwa wamama inasinga inasonga,
Inasonga mbele injili
inasonga mbele.
Kwa wababa inasonga; inasonga,
Inasonga mbele injili
inasonga mbele.
{Inasonga mbele injili, inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga
mbele.}x2
3. Kwa mapadri inasonga inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga mbele.
Kwa watawa inasonga; inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga mbele.
{Inasonga mbele injili, inasonga,
Inasonga mbele injili inasonga
mbele.}x2

2. LITURGY OF THE WORD

Somo la Kwanza

Kumbukumbu la Torati 6:3-9

“Umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote.”

Somo katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati. Musa aliwaambia watu, “Basi, ewe Israeli, ungeweza kusikiliza, kushika na kutenda yale yatakayokuletea heri na kuongezeka, jinsi Bwana Mungu wa baba zako alivyokuahidia, akikuwekea nchi ijaayo maziwa na asali.
Sikiliza, ee Israeli! Bwana Mungu wetu, ndiye Bwana peke yake! Umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote.
Maneno hayo ninayokuagiza leo yawe moyoni mwako. Uwafundishe wanao ukaapo nyumbani mwako, utembeapo njiani; uketipo na usimamapo. Uyafunge mkononi mwako iwe alama, mbele ya uso wako kama utepe. Uyaandike juu ya nyumba yako na juu ya milango yako.”
Neno la Bwana.

Zaburi

Zaburi 128:1-2, 3, 4-5 (K. Ja)

K. Heri kila mtu amchaye Bwana.

Heri kila mtu amchaye Bwana aendaye katika njia za Mungu. Hakika utakula matunda ya kazi ya mikono yako; utaona heri na kwako kutakuwa kwema.

K. Heri kila mtu amchaye Bwana

Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako, wanao kama machipukizi ya mizeituni, wakiizunguka meza yako.

K. Heri kila mtu amchaye Bwana

Ndivyo anavyobarikiwa yule amchaye Bwana. Bwana na akubariki toka Sioni, na uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako.

K. Heri kila mtu amchaye Bwana

Somo la pili

Warumi 8:26-30

“Walioadilishwa aliwapa pia utukufu wa mbinguni.”

Somo katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi

Ndugu: Roho anausaidia udhaifu wetu. Hatujui jinsi inavyotubidi kusali. Roho mwenyewe anatuombea sisi kwa maombi yasiyo- semeka.
Lakini Mungu achunguzaye mioyo ajua nia ya Roho anayewaombea watakatifu kwa Mungu. Twajua ya kuwa wale wampendao Mungu hufanikiwa yote, ndio wale walioitwa toka mwanzo katika azimio lake. Maana wale aliowajua toka mwanzo, aliwachagua toka mwanzo ili kuwalinganisha na sura ya Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua toka mwanzo aliwaita; nao aliowaita aliwapa uadilifu; nao walioadilishwa aliwapa pia utukufu wa mbinguni.

Neno la Bwana.

Shangilio

Mathayo 23:11, 126

K. Aliye mkubwa miongoni mwenu na awe mtumishi wenu, asema Bwana; na kila ajinyenyekeshaye atakuzwa.

Injili

Mathayo 11:25-30

“Haya umewaficha wenye hekima na busara, ukawafunulia watoto wachanga.”

*Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Mathayo

Wakati ule: Yesu alisema, “Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa haya umeyaficha wenye hekima na busara, ukawafunulia watoto wadogo. Ndivyo,
Baba, ilivyokupendeza. Nimekabidhiwa yote na Baba yangu. Hakuna amjuaye Mwana, ila Baba. Wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana na yeyote, ambaye
Mwana apenda kumfunulia. Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mzigo, nami nitawapumzisha. Mjitwike nira yangu na kujifunza kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtazipatia nafsi zenu raha. Kwani nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” Injili ya Bwana.

3. RITE OF PROFESSION

  •  Calling of Candidates
  • Presentation of the Candidates
  • Homily.

4. PROFESSION OF SOLEMN VOWS

· Examination of candidates
· Litany of the Saints
· Prayer

LITANIA YA WATAKATIFU

Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie. x1
Kristu utuhurumie Kristu utuhurumie. x1
Bwana utuhurumie Bwana utuhurumie. x1
Maria Mtakatifu Mama wa Mungu- Utuombee
Mtakatifu Mikaeli- Utuombee.
Watakatifu Malaika wa Mungu–
Mtuombee
Mtakatifu Yosefu- Utuombee
Mtakatifu Yohane Mbatizaji–
Utuombee
Watakatifu Petro na Paulo-
Mtuombee
Mtakatifu Andrea– Utuombee
Mtakatifu Yohane- Utuombee
Mtakatifu Maria Magdalena–
Utuombee

Mtakatifu Stefano- Utuombee.
Mtakatifu Laurenti– Utuombee
Mtakatifu Inyasi wa Antiokia –
Utuombee.
Mtakatifu Anyesi– Utuombee
Watakatifu Perpetua na Felisita-
Mtuombee.
Mtakatifu Gregori– Utuombee
Mtakatifu Agostino- Utuombee.
Mtakatifu Atanasi– Utuombee
Mtakatifu Basili – Utuombee
Mtakatifu Martino — Utuombee
Mtakatifu Benedikto – Utuombee
Watakatifu Fransisko na
Dominiko– Mtuombee
Mtakatifu Fransisko Saveri-
Utuombee.
Mtakatifu Yohana Maria Viane–
Utuombee

Mtakatifu Teresia wa Avila-
Utuombee
Mtakatifu Katerina wa
Siena- Utuombee
Mtakatifu Yosefati- Utuombee
Mtakatifu Calisto- Utuombee
Mtakatifu Cecilia- Utuombee
Mtakatifu Antonio wa Padua–
Utuombee
Mtakatifu Simeoni- Utuombee
Mtakatifu Bernado- Utuombee
Mtakatifu Klara- Utuombee
Mtakatifu Yosefu Kupertino –
Utuombee
Mtakatifu Maksimiliano
Maria Kolbe– Utuombee
Mtakatifu Katerina wa Alekzandria-
Utuombee
Mtakatifu Yohanne Paulo wa pili-
Utuombee
Mtakatifu Mathias- Utuombee
Mtakatifu Gabrieli- Utuombee
Mtakatifu Karoli – Utuombee
Mtakatifu Samueli- Utuombee
Watakatifu wote wa Mungu-
Mtuombee
Utuhurumie- Utuokoe Bwana
Katika uovu wowote-
Utuokoe Bwana

Katika dhambi yoyote-
Utuokoe Bwana
Katika mauti ya milele-
Utuokoe Bwana
Kwa kujifanya mwanadamu-
Utuokoe Bwana
Kwa kufa na kufufuka kwako
Utuokoe Bwana
Kwa kumtuma Roho Mtakatifu
Utuokoe Bwana
Sisi wakosefu- Twakuomba utusikie
Upende kulisimamia na kulilinda
Kanisa lako Takatifu-
Twakuomba utusikie.
Upende kumlinda Baba Mtakatifu
na wote wenye daraja katika dini
takatifu- Twakuomba utusikie.
Upende kuyajalia mataifa yote
amani na mapatano ya kweliTwakuomba utusikie
Upende kutudhibitisha sisi na
kutudumisha katika utumishi wako
mtakatifu- Twakuomba utusikie.
CHOIR:
Yesu Mwana wa Mungu aliye hai.
Twakuomba utusikie.
Kristu utusikie Kristu utusikie.
Kristu utusikilize Kristu utusikilize

5. OFFERTORY COLLECTION

SADAKA YANGU
@ Fr. A. Kauki

Sadaka yangu, kwako ewe
Mungu. Ni moyo mnyofu na
uliopondeka.
Tazama wapendezwa na kweli
ya moyo. Nawe wanijulisha
hekima kwa siri.
Nioshe kabisa na uovu wangu.
Na kinywa changu kitanena sifa
zako.
1. Maana wewe Bwana hupendezwi
na
dha-bihu za kuteketezwa.
Ama- sivyo mimi ningalikutolea
2. Wapendezwa na dhabihu za haki
Kuto-ka- kwa moyo mnyofu.
Zitolewazo juu ya madhabahu
yako.
3. Ee Mungu wa wokovu wangu.
Unipe moyo radhi wa utii.
Usiniondolee Roho Mtakatifu

NIKURUDISHIE NINI
(By Samson)

(Nikurudishie nini Bwana
kikupendeze.) x2
Kila ninachokitoa,
naona bado kidogo,
Nikurudishie nini Bwana
kikupendeze.
1. Nashika mfuko wangu,
Nakuta Kuna kidogo,
Naomba unipokee.

2. Ninakutolea Baba,
Zawadi hii ya fedha,
Naomba unipokee.
3. Nakutolea nafaka,
Kazi ya mikono yangu,
Naomba unipokee.
4. Ni mangapi nayafanya,
Wewe wanihurumia,
Ee Baba najiuliza.
5. Umenilinda mzima,
Kwa wiki iliyopita,
natoa shukrani zangu.

NGAI NIARITURATHIMAGA

Ngai niariturathimaga, rathime
mawira maitu; twamutegera na
wendo.
[TEN: Mawira maitu] arathime
Migunda itu,
twamutegera na wendo. x2
[Wee Ngai witu]
1. Niegutuhe kiria giothe
twamuhoya –
twamutegera na wendo.
Nigutuhe buthi wa irio na
mahiuMawira maitu na momone
umithio2. Mirimu itu yothe niegutohonia –
Twamutegera na wendo.
Atwehererie mogwati mawira-iniMabiacara maitu magithereme-

3. Ririra twahanda agatuma
tugetheTwamutegera na wendo.
Thuthi mbuca na menyiatwehererieNgaragu gwitu igutuike rugano

TWENDE WOTE ASTE ASTE
(Fr. Robert Onyonka)

Twende wote aste aste,
na sadaka mikononi,
Vipaji mbalimbali
twende wote kwa furaha.
Muumba wetu atubariki,
muumba wetu atuongoze,
Na tuseme aleluya, daima na
milele.
1. Mungu Baba tubariki,
Mungu mwana tukumboe.
Naye Roho mtakatifu
atuongoze daima.
2. Sadaka zetu mikononi,
matoleo kwa Baba,
Vyote vyako Mungu wetu
tubariki daima.
3. Watoto wetu twatoa kwako,
kufanya kazi yako Mungu,
Watoto wako Mungu wetu
Wabariki daima.

4. Mali yote yatoka kwako,
mifugo mimea pia kwako,
Twasema asante Mungu wetu
usifiwe daima.
5. Amka dada usiachwe nyuma,
sadaka yako mikononi,
Ili uchote Baraka tele –kwake
muumba wetu.
6. Ingawa Baba ni kidogo, pokea
zawadi zetu,
tumetoa kulingana na – uwezo
wetu.

SALA YANGU

(Sala yangu na ipae mbele yako
(na ipae)
kama moshi wa ubani.) x2
1. Ee Bwana upokee sadaka yetu,
tunayokutolea
kama shukrani zetu,
Ee Bwana pokea.
2. Ee Bwana upokee dhabihu zetu,
tunayokutolea
kutoka mashambani,
Ee Bwana pokea.
3. Ee Bwana upokee pia nia zetu,
tunazokutolea
kwa moyo wetu wote,
Ee Bwana pokea.

6. LITURGY OF THE EUCHARIST

HOLY HOLY – (CTK)
Holy holy – Holy holy (holy)
holy holy holy Lord of hosts. (x2)
Heaven and earth – Heaven and
earth,
heaven and earth are full of your
glory. (x2)
(Hossana) hosanna in the highest,
(hosanna) hosanna in the highest. (x2)
Sop: Blessed is he- All: blessed is
he, blessed is he who comes in the
Lord’s name. (x2)
(Hossana) hosanna in the highest,
(hosanna) hosanna in the highest.(x2)
Ee Bwana tunatangaza Kifo chako.
a kutukuza, ufufuko wako,
(mpaka utakapo kuja.) x2

NI AMANI KATIKA YESU BWANA
(Ni amani katika Yesu Bwana; ni
amani.) x2
1. Ni upendo…
2. Ni neema…
3. Ni huruma…
4. (Ni fadhili katika Yesu Bwana;
ni fadhili.) x2
5. Ni hekima…
6. Ni shukrani…

7. Ni furaha…
8. (Ni uchaji katika Yesu Bwana;
ni uchaji.) x2
9. Ni uwezo…
10. Ni ukweli…
11. Ni kusali….

LAMB OF GOD

1. Lamb of God who takes away
the sins of the world
have mercy on us.
2. Lamb of God who takes away
the sins of the world
have mercy on us.
3. Lamb of God who takes away
the sins of the world
oh grant us peace.

HOLY COMMUNION

MEZANI PAKE TWENDENI

1. Nakukaribisha Yesu wangu Ukae
moyoni mwangu. (Bwana) Nakukaribisha Yesu wangu Kinywaji chenye uzima.
Nishibishe Unishibishe
Kwa chakula Chakula cha uzima.
Uninyweshe kinywaji Ninyweshe
kinywaji Kinywaji safi cha roho.

2. Mwili wako ni chakula kinacho
iburudisha roho yangu. Yesu
karibu moyoni mwangu ukae
nami daima.
3. Damu yako ni kinywaji kinacho
iburudisha roho yangu. Yesu
karibu moyoni mwangu ukae
nami daima.
4. Kwa mwili na damu yako Ee
Yesu tunapata uzima tele. Yesu
karibu moyoni mwangu ukae
nami daima.

ZAWADI TOSHA
Mezani pake twendeni wote
Tukampokee ametualika. (x2)
1. Mwili wake ni chakula kweli
damu yake kinywaji safi.
2. Alaye mwili na kunywa damu
ana uzima wa milele.
3. Mbele ya kwenda tujitakase tutastahili kumpokea.
4. Karibu Yesu ukae nasi njia zako
utufundishe.
5. Na mwisho tufurahie nawe katika utukufu wako.

ZAENI MATUNDA

1. Zaeni matunda mema, zaeni
matunda yale,
zaeni yenye Baraka, zaeni ya
heri.
Bwana akiyapokea,
yatabarikiwa vyema;
Zaeni matunda mema,
zaeni ya heri.
2. Safisha mwenendo wako,
safisha matendo yako;
safisha na Bwana Yesu, safisha
yote.
3. Fanyeni kazi kidugu,
fanyeni kazi kwa bidi;
fanyeni na Bwana Yesu, fanyeni
yote.
4. Tolea matunda yako,
pamoja na moyo wako;
naye Bwana, Mungu wako,
atakubariki.
5. Baraka za Mungu Baba,
baraka za Mungu Mwana,
na za Roho Mtakatifu, ziwe
nanyi nyote.
6. Bwana akiyapokea,
yatabarikiwa vyema;
Zaeni matunda mema,
zaeni ya heri.

 

Details

Date:
August 17
Time:
9:30 AM - 5:00 PM
Event Category: